Wednesday, May 25, 2011

TAARIFA YA KITABIBU YA KILICHOSABABISHA VIFO VYA WANANCHI TARIME

Na. Grayson Nyakarungu

Nafahamu nyote mwajua tukio la Tarime, la wananchi kuuwawa na jeshi la polisi huko migodini Nyamongo Wilayani Tarime,tarehe juma lililopita.

Wafiwa wallitaka kujua undani wa mauaji ya ndugu zao, ili waweze kufuata njia za kisheria za kudai haki yao ya kisheria.

Ililazimika uchunguzi wa kitaalam ufanyike ili ukweli ujulikane...

Uchunguzi huu ulifanywa jana na mtaalam wa uchunguzi wa aina hii (Post Motum) ya kitaalam, Dr Makata kutoka wizara ya afya kitengo cha dharura matukio tata.

Kwa upande wa wafiwa waliwakilishwa na Grayson Nyakarungu, aliyepewa imani na chama pia kuhakikisha ukweli ndio unaletwa hadharani.

Pia jeshi la polisi na Hospitali ya wilaya ya Tarime walikuwa na wawakilishi wao.

Tuliifanyia miili mnne kati ya mitano, ya watu walio uwawa, kwani mwili mmoja ulishazikwa kwa kuibiwa na polisi.

IFUATAYO NI TAARIFA HALISI TULIYOTOKA NAYO BAADA YA UCHUNGUZI WA WETU, KWA KULINDA NA KUHESHIMU UADILIFU WA TAALUMA YETU YA KIAFYA.

KIAPO NILICHOAPA HUKO CHUONI (MEDICAL ETHICS)

1. Kile kinachoonekana katika vipimo/uchunguzi, ndicho kinachotakiwa kuwekwa wazi kwa muhusika.

2. Sitakeuka wala kughiribu utu wa mtu kwa sababu zozote zile.

Hizo ni chache tu kati ya Medical Ethics nyingi, ambazo niliapa kuzilinda na kuzisimamia.

POST MORTUM ROOM

Tulianza kazi hii saa 10:25 A.M hadi saa 16:57 P.M baada ya wafiwa kuitambua miili ya ndugu zao.

1. Mwili wa Emmanueli Magige

P.M No 1-5-11

T.G.H

Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto wa juu ya nyonga)

Wound size: 0.5 cm diameter the wound was round.

Exit site: Lumber region back (juu ya kiuno kidogo karibu na uti wa mgongo)

Wound size: 2.5 cm diameter

Positive findings;-

-Blood vessels/Nerves and sorounding muscles were destroyed.

-The clavicle bone was destroyed and blood clots was seen, ( mfupa mkuu wa kiuno na nyonga uliharibiwa na damu nyingi ilivuja na imeonekana imeganda humo)

But beneath the exit site, there was a cut wound, 2.5 cm diameter.

Lakini kulikuwa na alama ya jeraha kubwa linaloonyesha alama ya kuwa kitu chenye ncha kali kilichoma, na hii ilileta hisia tofauti, polisi walihisi kuwa aliangukia jiwe au kijiti kilichomchoma, kwa hili tulibishana na tukaamua hakuna jibu la nini kilichoma, ila mimi nilihisi na kusimamia kuwa alichomwa na singe ya bunduki, na ndipo niliomba nguo zake zitafutwe ili tuzichunguze na tubaini ukweli, hata hivyo hazikupatikana.

2. Mwili wa Chacha Ngoka

P.M No. 2-5-11

T.G.H

Entrance site: Right side of the body back 16 cm from illiac (usawa wa bega chini na juu ya kiuno, nyuma ya mwili.

Wound size: 0.3 cm diameter

Exit site: In 5th intercoastal muscle right side, 2cm from the nipple.

Wound size: 5cm diameter

Positive findings

Major blood vessels were destroyed

Midle and right lobe of liver were destroyed led to rasaration

In the Trachea, blood clot was seen.

3. Mwili wa Chawali Boke.

P.M No. 3-5-11.

T.G. H

Entrance site: Occipital bone 8cm from the Pinna, (Kisogoni sm 8 kutoka sikio la kushoto)

Wound size: 0.2 cm diameter

Exit site: In parietal bone ( kwenye paji la uso pembeni kidogo)

Wound size: 5cm diameter

Positive findings;-

The brain and inner part of the head was destucted, blood clotts was seen, this was due to blood aspiration.

4. Mwili wa Mwikwabe Marwa Mwita

P.M No. 4-5-11

T.G.H

Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto juu ya nyonga)

Wound size: 3.5 cm diameter

Exit site: It was not pass through, it remained intact.

Wound size: None

Positive findings;-

There was worse destruction of;-

-Femoral artery

-Femoral vein

-Sorrounding muscles

- Fructure of illiac bone ( mfupa wa nyonga na uzazi)

- Piece of lead was seen lying deeply inpsoas muscle, sorrounded by bone fragments

Msimamo wangu kimaadili na na kibinadamu;-

1. Polisi walikusudia kuua na sio kudhibiti watu waliowaita wavamizi, kwani kwa mjibu wa force law, hawakutakiwa kupiga risasi sehemu yoyote tofauti na miguuni.

2. Polisi waliwapiga risasi watu waliokuwa wakikimbia kutoka eneo hilo, kwani risasi zote zimepenya kwa upande wa nyuma wa mwili na zikatokea upande wa mbele wa mwili.

HIVYO wananchi hawa hawakupambana na polisi, bali walipigwa risasi wakiwa wanakimbia, ndio sababu ya risasi zote kuingia sehemu za nyuma za miili yao.

Mungu watazame waja wako na uwalinde na yote aliyoyaandaa SHETANI.

MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI AMINA, NITAKUWA SHAHIDI MWEMA NA MSEMA UKWEI KWA KUUENZI UTU.

No comments: