Friday, May 20, 2011

SHEIKH YAHYA HUSSEIN NA MZEE ATHUMAN MWINYIMVUA WAFARIKI DUNIAYule mtabiri na mnajimu maarufu wa Afrika Mashariki ya kati Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia mnamo majira ya saa nne asubuhi hii nyumbani mwake Mwembechai jijini Dar es Salaam. Sheikh huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya ugonjwa wa Moyo. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za vyombo vya habari maziko yatarajiwa kufanyia kesho nyumbani kwake.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Athuman Mwinyimvua amefariki dunia. Mzee Mwinyimvua alikumbwa na umauti wake leo nyumbani mwake Magomeni Mwembechai. Taarifa zaeleza kwamba maziko yatarajiwa kufanyika leo alasiri .

MUNGU ZAIWEKE ROHO ZAO MAHALI PEMA PEPONI AMEN.

No comments: