Friday, April 29, 2011

MJUKUU WA MALKIA WA UINGEREZA ATARAJIWA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA LEO
Picha maalum ya Prince William na mkewe mtarajiwa Kate Middleton


Leo ni leo ambapo mjukuu wa malkia wa Uingereza Prince William ambaye inaelezwa kwamba yuko katika mlolongo wa urithi wa kiti cha Ufalme cha Uingereza anapofunga pingu za Maisha na mchumba wake wa siku nyingi Bi Kete Middleton. Chereko chereko na shamrashamra za vyombo vya magharibi zimeshamiri katika jiji la London katika maeneo ya Goring hotel ambapo Kate ameutumia usiku wake akiwa na wazazi wake Westminster Abbey ambapo ndoa yao itafungwa na Buckingham Palace yalipo makazi ya Malkia ambapo baada ya ndoa yao watakwenda kusheherekea hapo. Kama ilivyo katika tamaduni zao Prince William na Kate watatoka nje ya Buckingham Palace mara baada ya kufunga ndoa kidirishani na kuwapungia mashabiki huku akimpiga busu la nguvu mkewe Kate kama alivyofanya baba yake kwa marehemu mama yake Princess Diana.

Inaelezwa kwamba Kate ni msichana ambaye ametoka katika familia ambayo si ya kikabaila kwani katika nchi ya Uingereza bado kuna mabaki hayo na makabaila hao huwa na mahusiano ya karibu na familia ya kifalme ama kuwa katika mlolongo mrefu katika uhusiano na koo ya kifalme kinyume na ilivyokuwa kwa mama yake William Princess Diana.

Listi ndefu ya wageni inatarajiwa ambapo wapo wale ambao wana ukaribu na mjukuu wa kifalme na wale ambao wana mahusiano ya muda mrefu ya kifamilia pamoja na familia za kifalme huko ulaya. Kwa ufupi tu muogeleaji maarufu ambaye ni rafiki wa William bwana Ian Thorpe wa Australia anatajwa kuhudhuria,Malkia Magreth wa Denmark, Prince Pavlos wa Ugiriki na mkewe, Malkia Sofia wa Uhispania na wanawe Prince Felipe na mkewe, Mfalme Harald wa Norway na mkewe listi ni ndefu .

Inaelezwa kwamba ni utamaduni wa ndoa nyingi za kifalme hasa Uingereza kufungwa katika jumba la Westminster Abbey na anayeoa au kuolewa ili arithi kiti cha ufalme ni lazima awe Muanglikana sio mkatoliki. Utamaduni ambao unaelezwa ulianza tokea mwaka 1066. Blogu hii inawatakia maisha marefu mjukuu wa Malkia pamoja na mkewe Kate Middleton katika maisha yao ya ndoa.

No comments: