Friday, April 1, 2011

BABU WA LOLIONDO KULETA KIKOMBE DAR

Baada ya manung'uniko ya muda mrefu kuhusiana na matatizo ya miundombinu yanayosababishwa na mvua pamoja na uwingi wa watu katika kijiji cha Samunge wilayani Loliondo, hatimaye serikali imeamua kumjengea mchungaji Ambilikile Mwasapile kituo maalum cha kutoa tiba jijini Dar es Salaam. Akieleza hayo mratibu na mwandamizi kutoka kitengo cha tiba asilia wa Wizara ya Afya, alielezea hatua hiyo itawarahisishia wananchi wengi kupata huduma ya kikombe pamoja na wageni sanjari na wao kurahisisha tafiti zao.

Hatua hii imekuja baada ya mchungaji huyo kuzidiwa na wagonjwa na kupelekea kusitisha kwa watu kuja Loliondo kwa wiki moja ili aweze kumalizia kuwapatia huduma ya vikombe wale wliobakia. Wakati huo huo Mchungaji Ambilikile ama Babu ameelezea dawa hii inatibu magonjwa mengi kama vile kansa, ugumba na inaweza kukufanya ukawa kijana.

Alipoulizwa msemaji wa Wizara ya Afya kuhusiana na msururu wa watu wanaojitokeza kutoa huduma ya vikombe katika mikoa ya Mbeya na Tabora na serikali inachukulaje changamoto hiyo alisema kwamba wao wanafurahi kuona watu wanatoa huduma ya vikombe lakini ni lazima vifanyiwe utafiti na vipitie TBS kuthibitishwa kwa matumizi ya binadamu. Hata hivyo aliwapongeza na kuwashukuru kwa kuwapunguzia adha madaktari na manesi ya wagonjwa kwa wao kujitolea na kuahidi kufanya tathmini ya kina endapo watoa vikombe hao watajumuishwa na Babu jijini Dar.

NAWATAKIENI NYOTE SIKU NJEMA YA WAJINGA

No comments: