Wednesday, March 2, 2011

MAHAKAMA YA NDIZI - MABIBO YAVUNJWA

Kwa wale wakazi wa maeneo ya Ubungo, Shekilango, Urafiki, Manzese-Chama na Mabibo, Wazee wa Big Bon watakuwa wanaijua vizuri mahakama ya ndizi. Leo kulikuwa na kimbembe baina ya wachuuzi na watu wa Manispaa ya Kinondoni na kupelekea polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia kuitwa. Sasa itabidi watu waende Kariakoo shimoni. Mahakama ya ndizi iliweza kuwainua kimapato watu wengi kuanzia wakulima, wachuuzi, madalali, makuli, wauza mabaa mpaka walaji wa kawaida.

No comments: