Wednesday, March 9, 2011

LEO NI SIKU YA JUMATANO YA MAJIVU

Leo ni siku ya jumatano ya majivu. Siku hii ni siku mahsusi kwa wakristo ambapo ndio maadhimisho ya siku ya Kwaresma ambapo kilele chake ni sikukuu ya Pasaka. Inaelezwa kwamba Masiya Yesu Kristo alifunga kwa siku 40 kabla ya kujaribiwa na shetani. Hivyo basi Wakristo wote katika siku hizi 40 wanaaswa kufunga , kutubu na kumrudia Mungu wao. Wakristo hupakwa majivu kama ishara ya maombolezo, majuto ya dhambi zetu lakini pia tunairejea ahadi ya Mungu aliyowaambia Adam na Eva baada ya kuvunja agano kwamba watarudi mavumbini.

Tuitumie siku ya Kwaresma kwa kufunga , kujutia dhambi zetu na kuwaombea viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuiongoza nchi yetu wasije wakaipeleka katika maafa na mgawanyiko kama jinsi inavyoelekea. Pia tuziombee jamii zetu, rika zote, dini zote wake kwa waume ili wamrejee Mungu wao ili wairithi pepo na waishi maisha ya raha na maadili.

KWARESMA NJEMA KWA WAKRISTO WOTE

No comments: