Thursday, March 24, 2011

KIMARO: UVCCM NI BUA LILILOKAUKADaniel Mjema, Moshi

MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Vunjo na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Aloyce Kimaro ameushambulia Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) akisema umepoteza mvuto huku akiufananisha na bua lililokauka linaloweza kusukumwa na upepo.

Kimaro alisema hayo jana mjini hapa na kusisitizakuwa ameamua kujitokeza hadharani kutoa maoni yake akiwa mwanachama wa CCM. Alisema umoja huo unastahili kubeba lawama kutokana na vijana wengi kuamua kukiunga mkono chama cha upinzani cha Chadema.

“UVCCM hauna nguvu tena, hivi wanataka viongozi wa CCM wawaogope kwa lipi? Hawana ushawishi tena kama wana nguvu waende UDSM (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) kama kuna vijana watawasilikiza,” alisema Kimaro.
Kimaro alihoji UVCCM kilikuwa wapi muda wote wakati Serikali ya CCM ikihusishwa na ufisadi na kuongeza kuwa walipaswa kujitokeza wakati huo na kujibu mapigo, ikiwamo kuwataja wale wanaokipaka matope.

“Leo baada ya mambo kuharibika ndiyo wanajitokeza, hivi jamii itawaaminije kama hawatumiwi na mafisadi? Tungewaona wako makini kama wangekuja na mkakati wa kuiimarisha CCM kabla ya 2015 na siyo kupayukapayuka tu,” alisisitiza.

Kimaro alisema kitendo cha kumshambulia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ni cha utovu wa nidhamu kwa sababu heshima ya Sitta mbele ya jamii ya Watanzania ni mara dufu ya heshima ya umoja huo.

Mbunge huyo wa zamani ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu, alisema Sitta alipokuwa Spika wa Bunge alionyesha uzalendo wa dhati kwa nchi yake kwa kuongoza mijadala iliyokuwa na maslahi ya nchi... “Kupayuka payuka leo na kuwashumbulia viongozi wa kitaifa wa CCM na hata kuwapa ultimatum (ukomo) wa kuchukua hatua ni sawa na kumtisha mtu mzima kwa picha ya nyau (paka).”

Kimaro alimtaka Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malissa na kundi lake kuacha kujifurahisha kwa kutoa matamko ambayo jamii haiyasikilizi na badala yake waweke mikakati ya kuurudishia heshima umoja huo.“UVCCM sasa hivi inamwakilisha kijana gani hapa nchini? Vijana wote wamekimbilia Chadema huku umoja huo ukitazama, halafu leo wanajifanya kumtafuta mchawi… waache usanii waje na mikakati,” alisitiza Kimaro

MWANANCHI

3 comments:

Shaaban said...

I like your blog and read it often. Lived in Mtwara for a couple of years. Hope all is well and keep writing.
cheers!!!
Fundi

Shaaban said...

check www,habari-za-kibogoji.com

Baraka Mfunguo said...

Thanks Shaaban. You are warmly welcome