Friday, February 18, 2011

WADAU WA CLOUDS MEDIA WASHIRIKI UCHANGIAJI WA DAMU KWA AJILI YA WAHANGA WA GONGO LA MBOTO.

Mshauri nasaha wa mpango wa taifa wa damu salama kanda ya mashariki akimpima mapigo ya moyo mdau wa Clouds Media
Wadau wa Clouds Media wakiwa vitandani tayari kwa zoezi la uchangiaji damu kwa hiyari
Hata wakina dada nao hawakubaki nyuma . Janga la Gongo la Mboto limewagusa watu wengi kwa kiasi kikubwa
Mtangazaji mwandamizi wa Clouds Media akipimwa kiwango cha damu kabla ya kwenda kwa mshauri nasaha


PICHA KWA HISANI YA MICHUZI JR WA BLOGU YA JIACHIE

My Take:
Pongezi kwa wadau wa Clouds Media mmeonyesha njia kwa kupitia chombo chenu cha habari sio kwa kuchangia damu pekee, bali mmewatia hamasa hata wale ambao walikuwa hawaoni umuhimu wa kuokoa maisha ya wengine. Pongezi nyingine ziwafikie wadau wa Mpango wa Damu Salama ambao kazi yao ni kuhakikisha mwananchi anapata huduma ya damu pale anapohitaji kwa wakati bila gharama yoyote narudia DAMU HAIUZWI.

No comments: