Wednesday, January 12, 2011

MBILIA BEL-SANS FRONTIERE NA TIKA BAZUWA

Mbilia Bel ni Mwanamama Mkongwe na mrembo katika tasnia ya muziki wa Rhumba. Mwanamama huyu huwa ananigusa sana katika miziki yake hii japokuwa sielewi anaimba nini lakini naweza kuburudika nafsi kwa mpangilio mzuri wa muziki pamoja na Sauti yake nyororo. Kipaji cha Mwanamama huyu kilianzia kwa Abeti Maskini na Kufikia kilele akiwa Afrisa International akiwa na Tabu Ley "Rocherau" ambaye walifunga ndoa ya kukata na shoka wakiwa katika ndege (hewani). Lakini katika maisha ndio hivyo tena.

Mzee Tabu Ley akazidiwa kete na kupelekea yeye kulazwa hospitali kwa shinikizo na mstuko wa kuachwa na mpenziwe (Kwa kweli inauma) na yeye kutunga wimbo. Pata Vibao Vya" Sans Frontiere" na "Tika Bazuwa" vilivyopo katika Albamu yake ya "Phenomene" kazi ya Rigo Star (mpangilio wa sauti na vyombo) na Frank Curier ambaye ni mtunzi .


Hii Albamu ilikamata vilivyo enzi hizo sio mchezo huyu mwanamama kwa kweli ni mrembo na bado moto wa kuotea mbali achilia mbali kwamba umri wake ni mkubwa

BLOGU HII INAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA MAPINDUZI KWA RAI YA KUDUMISHA AMANI. KAMWE KUMWAGA DAMU SIO SULUHU YA MATATIZO YETU. TUSHEHEREKEE PIA TUKIKUMBUKA NA KUOMBOLEZA WALE WALIOPOTEZA MAISHA YAO KUTOKANA NA TUKIO HILI LA KIHISTORIA. TUYATUKUZE MAPINDUZI KAMA DHANA YA UKOMBOZI NA KAMWE SI MATOKEO YAKE.

No comments: