Friday, January 7, 2011

MAONI YA MDAU KUHUSU BANDIKO LA MWANAKIJIJI LA UDINI NA CHUPA YA POMBE

Mwana kijiji hakika umeweka vidole vya tiba katika donda ndugu kwa makala hii ambayo sidhani kwa wananchi wengi wa Tanzania wanaweza kufaidika nayo, na sababu ya kutofaidika nayo ni kutokana na kile ulichokiita(UJINGA WA KIDINI.

Kwa kuongezea maoni yangu mimi naona ujinga huu unatokana na sisi waafrika au sema mataifa ya kiafrika ambayo yaliyoletewa hizi dini kuu mbili za kigeni UISILAMU NA UKRISTO na kuzikumbatia kwa ujinga hii ukiongezea pia ajenda za nje za waleta dini zenyewe ambazo pia wanachangia kutufarikisha na kutuongezea ujinga mpaka kufikia kuwa na akili au mawazo mgando, kwa hoja au madai kwamba ni dini gani ya kweli na sahii na dini gani si ya kweli na potovu.

kuna ukweli mwingine wa wazi na usiojificha kwamba kanisa kuu la katoliki ni dola juu ya wakristo wote duniani na linakua na ajenda mbalimbali kwa waumini wao na hasa kuhakikisha kuwapandikiza wakatoliki katika nafasi zote za ngazi za juu ikiwemo urais na kwa vile waislamu hawana utaratibu wa Msikiti mkuu wa kuwatawala waislamu wote duniani,kama wakatoliki utakuta mataifa haya mawali ya kislamu Saudi Arabia na Irani hujenga na kueneza mtafaruko wa waislamu wenyewe kwa wenyewe kimadhebu na kisiasa mafano wa swala ya Eddi daima uswaliwa kwa udini wa kisiasa badala ya kusali kitaifa kwa wana dini moja hiyo.Hii hukiongezea kwamba wakati huohuo mataifa hayo huwa yanapigania kuhakisha waislamu wanashika nafasi za ngazi za juu kimadaraka ikiwemo urais.

Sasa kwa tatizo kuu la ujinga wa kidini ambalo umelichambua kwa kirefu wataalamu au viongozi wa dini hizi mbili kuu aidha kwa ujinga wao wa kidini au kwa kutekeleza ajenda za kanisa kuu la katoliki au ajenda ya Saudi Arabia au Irani tunajikuta nchi zetu daima tunaukumbatia huu ujinga wa kidini.

Kama ujuavyo daima wanasiasa wanatumia mbinu zote zile za halali na zisizo za kihalali ili wafike madarakani na daima huitumia dini au waumini wa dini zao ziwafikishe madarakani.
Utakumbuka Mwalimu Nyerere,baba wa taifa letu alieipenda nchi yake na wananchi wake alituhumiwa kwamba anawapendelea wakristo eti kwa sababu tu yeye ni mkristo tena wa mkatoliki huo ulikuwa ni ujinga wa kidini wa wafuasi wa kiislamu na kutulia moyo kwa wana dini ya kikristo.Na kwa kusisitizia zaidi ujinga wa wataalamu wetu wa dini hizo mbili pale mwalimu aliposema moja ya tamko lake mashuhuri kwamba''TANZANIA HAINA DINI,BALI WANANCHI WAKE NDIE WENYE DINI''Masikini,wafuasi na viongozi wa dini zote mbili hawakumuelewa mpaka alipowahutubia tena mapadri na masheikh kuwafafanulia msemo huo. kwa maana hiyo basi si wafuasi tu ni wajinga bali mpaka viongozi wao wa kidini ni wajinga wa udini.

Ebu mwangalie mwanasiasa kiongozi Rais wa awamu ya pili Hassani Mwinyi alikua msatari wa mbele kuuonyesha udini wake wakati yeye hakupaswa kufanya hivyo kwa vile alikuwa ni Rais wa nchi lakini amebaki kama ni Rais mwenye kuheshimiwa sana na waislamu kwa vile walimuona kma ni mkombozi wao kutokana na kukandamizwa kwa waislamu(kama wanavyodai)wakati wa utawala wa Baba yetu wa taifa Mwalimu Nyerere ambaye hakuwa kamwe mjinga wa udini wala kuitumia dini kwa masilahi yake kama mwanasiasa.

Mchango wangu katika tiba ya ujinga huu wa udini ni lazima kwanza viongozi wa kisiasa wawe msatari wa mbele na kuwa wakali na wenye kukemea ujinga huu wa udini na kutoitumia dini kwa masilahi yao ya kisiasa au kutumikia ajenda za nje za kanisa katoliki,saudi arabia au Irani.ushahidi wa wazi wa kulipuana mabomu na kuuana kila siku kwa wakareketwa wa ujinga huo wa udini hususa waislamu tunaziona na kuishi nazo duniani kuanzia pakistani,lebanoni,─▒raq na irani kumalizia tukio la kigaidi la kimataifa la Septemba 11 Amerika.

Wanasiasa hao wachukue msemo wa Mwalimu Nyerere baba wa taifa ndio mongozo na dira ya kwamba''Tanzania haina dini bali watanzania ndio wenye dini''kwa maana dini yako ni ya kwako wewe mwenyewe na Mungu wako una uhuru wa kuabudu unavyotaka bila kuingilia,kudharau na kukebehi dini au itikadi ya mtu mwingine hata kama anaabudu jiwe au mizimu.

No comments: