Wednesday, December 22, 2010

POLISI WAWADHALILISHA RAIA -ARUSHAJESHI la polisi mkoani Arusha, limekumbwa na kashfa nyingine, baada ya polisi wake wawili kutuhumiwa kuwateka vijana watatu waliokuwa wakifanyabiashara na kuwapora fedha na kuwalazimisha kujamiiana huku wakiwapiga picha katika eneo la Ikulu ndogo ya Arusha.

Tukio la aina yake, ambalo tayari limeripotiwa polisi, lilitokea juzi kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana na polisi kuwaachia huru. Vijana hao, walikuwa wakifanya biashara ya kuuza virutubisho vya mwili aina ya Arovela.


Wakizungumza katika ofisi za Mwananchi jana,wafanyabiashara hao, Victoria Agustine(22),Evance Fank(24) Godbless Shirima(18), walisema walikamatwa na polisi hao, wakiwa wanapita nje ya jengo la Ikulu ndogo ambalo lipo jirani na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.


Frank alisema wakiwa wanatembeza bidhaa hizo ambazo zinatolewa nakampuni ya Mwema General Supply ya Arusha, walipita mbele ya Ikulu, na polisi wawili walikuwa lindo waliwaita nawalipoingia ndani na Ikulu walianza kuwahoji maswali kuhusu biashara hiyo.


Alisema ghafla waliambiwa kupiga magoti na kuweka mikono juu, na kuanza kupewa mazoezi ya kupiga pushapu, kuruka kichurachura na baadaye waliwataka kuwakabidhi fedha zote walizonazo.


"Tulisema hatuna fedha, lakini mmoja alianza kutupekuwa na kuchukua Sh 200,000 za mauzo kwa kiongoziwetu Shirima,” alisema Frank.


Frank alisema pamoja na kuchukua fedha hizo, pia waliwataka kutoa sadaka na walichukua kwa nguvu Sh 2,500 kutoka kwa kila mmoja.


"Mimi nilikuwa nawaambia kama tumefanya makosa watupeleke polisi waligoma kabisa na walikuwa wakisisitiza tumefanya makosa kupita mbele ya Ikulu,"alisema Frank.


Alisema baaday waliwavua nguo na kuwataka kufanya mapenzi na Fank na Victoria waliambiwa kukubatiana nakunyonyana ulimi.


"Mimi nilikataa kufanya mapenzi wakanilazimisha huku, wakinipiga, lakini nilikataa na kulala ndipo walilazimisha tunyonyane ulimi na Victoria huku wakitupiga picha kwa simu ya mkononi,"alisema Frank.


Naye Shirima ambaye alikuwa kiongozi, alisema wakati wanapigwa alimtambua polisi mmoja na akamuita kwa jina huku akiomba wasiendelee kuwatesa, lakini aligoma na kuendelea kuwapiga.


"Tuliwakuta wamelewa na mimi namjua mmoja kabisa kwa jina(jina linahifadhiwa) nikamwambia mimi namjua na kaka yangu alikuwa polisi na pia kuna ndugu yangu ni ofisa wa Magereza Manyara, aliposikia hivyo alianza kunihoji ni wapi nilimuona nikamwambia ndipo alisema anatupeleka polisi, lakini tulipofikanjiani alituacha na kuondoka,"alisema Shirima.


Mwandishi wa habari hizi, juzi aliwakuta wafanyabiashara hao, wakiwa wanatoa maelezo katika ofisi ya Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha na baadaye kwa kamanda wa polisi mkoani Arusha, lakini hadi jana hakuna hatua ambazo zilikuwa zimechukuliwa.


"Yule mkuu wa upelelezi badala ya kufungua kesi ya malalamiko yetu alianza kuzungumza na kiongozi wa walinzi wa Ikulu na kuomba tukutanishwe ili waombe msahama na akatuomba tuache namba za simu lakini hadi leo(jana) hajatupigia,"alisema Shirima.


Vijana hao, wamelishauri jeshi la polisi kuchukua hatua kali dhidi ya polisi na kuwalazimisha kufuta picha walizowapiga ili zisisambaa mitaani.


Alifafanua kuwa baada ya kufika kwa kamanda wa polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye alitusikiliza na kutueleza kuwa atatupigia simu, lakini pia hadi leo (jana) bado hajatupigia.


Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye hakupatikana jana kuelezea tuhuma hizo, baada ya simu yake ya mkononi kupokelewa na msaidizi wake aliyedai kuwa yupo katika kikao ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha. Pia saa 8:52 Mwananchi lilimpigia tena lakini simu yake haikupokelewa na ilikuwa ikita tu muda wote bila kujibiwa.


Tukio hili ni mfululizo wa matukio ya unyanyasaji wa polisi kwa raia na hivi karibuni walituhumiwa kumpiga mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema na pia waliwahi kutuhumiwa kuwauwa kwa risasi vijana wawili eneo la Kijenge, lakini hata hivyo hakuna hatua zilizochukuliwa.


My take: Kama Andengenye ameshindwa kuwashughulikia polisi waliofanya unyanyasaji ule, Basi hatua kali zichukuliwe na IGP, Vinginevyo hata imani ndogo tuliyonayo dhidi ya polisi zitakuwa zimetoweka, tutaingia mtaani tukiwa tayari hata kufa kupambana na hili jeshi dhalimu la polisi.

No comments: